Posts

Showing posts from June, 2017

NI KWA NINI MAONO YAKO HAYAFANIKIWI?

Ndugu msomaji wa makala hii, huenda umewahi kujiuliza ni kwa nini unakuwa na maono lakini hayfanikiwi au hayatimii. Leo nataka tuzunguze kwa habari ya madhara yatokanayo na kuwaambia watu maono uliyo nayo kabla ya kuyaweka katika vitendo. Tutajifunza nini maana ya maono, faida ya kuwa na maono lakini pia tutajifunza madhara yatokanayo na kuwaambia watu maono yako kabla hayajatimia au hujayafanyia kazi. Nini maana ya maono? Yamkini umesikia hili neno maono lakini hujapata maana yake kamili. Maono ni picha ya mbeleni, malengo na mipango ambayo mtu anakuwa nayo na, ambayo atafanyia juhudi ili afikie au atimize. Malengo au mipango mtu anaipanga kwa siku zijazo au wakati fulani ulioko mbeleni ili kutekeleza, tunaweza kuichukulia kama maono mtu aliyo nayo. Kwa mfano, unataka baada ya miezi sita uwe na kiwanja cha kujenga nyumba au uwe na gari lako mwenyewe, hayo ni maono ambayo unatamani yatimie katika wakati huo. Hivyo tunaweza kusema kuwa hiyo ni picha yako ya mbe...

JE UNATAFUTA MTAJI?

       Rafiki yangu, je unatafuta mtaji ili ufanye biashara?  Au unafikiri kwamba ili uweze kufanikiwa au kufanya jambo fulani ni lazima upate mtaji kwanza au uwe na fedha ndipo uweze kufanya?. Haya ni mawazo ya walio wengi hata mimi niliwaza hivyo mara nyingi lakini sikuwa sahihi. Nilitumia muda mwingi na nguvu nyingi kutafuta mtaji ili nifanye biashara lakini nilijikuta napoteza muda mwingi bila kujua.                 Inawezekana hata wewe ni miongoni mwa watu wenye mwazo kama niliyokuwa nayo na huenda mpaka sasa hujapata mtaji, na hujui utapata kwa njia gani. Unaweza kusubiri ili upate pesa lakini wakati huo kama huna wazo (idea) utajikuta hakuna ulichokifanya na muda ukapoteza muda mwingi na hata ukija kupata pesa ile ukaitumia kwa matumizi yasiyo sahihi na ukaishia kwenye umaskini na hali ngumu ya maisha. Mtaji bila wazo ni sawa na kuwasha jiko wakati huna cha...

UKIACHA TABIA HII UTAWEZA KUTIMIZA MALENGO YAKO.

       Ikiwa unataka kufanikiwa katika mipango yako na kuweza kutimiza malengo yako katika wakati sahihi, tabia ya kuahirisha mambo yafaa uiache mara moja.Mara nyingi tunapenda kuahirisha mambo na kusema nitafanya baadaye au siku hali ikiwa nzuri. Ni vyema ujue kuwa hakuna siku nzuri ya kufanya jambo unalotaka kufanya isipokua umechukua hatua leo. Tabia ya kuahirisha mambo ni ugonjwa mbaya sana kwenye mafanikio au kwenye kufikia malengo yako.          Kama unataka kutimiza ndoto na mafanikio yako kwa ujumla, kuahirisha mambo ni tabia ya kwanza ambayo unatakiwa kuachana nayo mara moja. Wengi wamekuwa ni watu wa tabia hii ya kuahirisha mambo na kuona ni kitu cha kawaida au kitasaidia kufanya vizuri kumbe la hasha. Kwa mfano, utakuta mtu anataka kuanzisha jambo fulani labda ni biashara au mradi fulani, lakini katika hali ya kushangaza analiacha jambo lile na kudai kwamba atalifanya muda mwingine. Kuahiri...

JE, WAJUA KUWA MUDA UNAYOYOMA?

Mwanadamu anayo maswali mengi ya kujiuliza kuhusu wakati anaoishi hapa duniani tangu kuzaliwa hadi umri alionao. Mtu mwenye akili na ufahamu lazima atajiuliza na kujitathimini kuwa amefanya nini katika umri alionao akiwa ni kijana au mzee. Kama tunavyojua ya kuwa muda unakwenda kasi sana na kadiri siku zinavyosogea ndivyo maisha ya mwanadamu yanavyoelekea ukingoni.  Kuna wakati natafakari juu ya maisha yangu na muda nilionao hapa duniani  na kujiuliza maswali mengi kila iitwapo leo. Siku zinaenda, miaka inasogea na majira hayasimami, ni kama ilivyo dunia inavyojizungusha katika mhimili wake bila kupumzika tukapata kuuona usiku na mchana ndivyo muda unavyosogea au unavyoyoyoma. Lazima nijiulize nimefanya nini katika umri nilio nao tangu nimeanza kupata ufahamu aidha nimeutumia muda wangu kwa faida au hasara. Ni vyema kutambua kuwa kila siku ni siku mpya na siku hazifanani katika muda wa mwanadamu kuishi hapa duniani unapoamka asubuhi sio kama jana bali umekuwa ...