UKIACHA TABIA HII UTAWEZA KUTIMIZA MALENGO YAKO.
Ikiwa
unataka kufanikiwa katika mipango yako na kuweza kutimiza malengo yako
katika wakati sahihi, tabia ya kuahirisha mambo yafaa uiache mara moja.Mara nyingi tunapenda kuahirisha mambo na kusema nitafanya baadaye au siku hali ikiwa nzuri.
Ni vyema ujue kuwa hakuna siku nzuri ya kufanya jambo unalotaka kufanya isipokua umechukua hatua leo. Tabia ya kuahirisha mambo ni ugonjwa mbaya sana kwenye mafanikio au kwenye kufikia malengo yako.
Kama
unataka kutimiza ndoto na mafanikio yako kwa ujumla, kuahirisha mambo
ni tabia ya kwanza ambayo unatakiwa kuachana nayo mara moja. Wengi
wamekuwa ni watu wa tabia hii ya kuahirisha mambo na kuona ni kitu cha
kawaida au kitasaidia kufanya vizuri kumbe la hasha.
Kwa
mfano, utakuta mtu anataka kuanzisha jambo fulani labda ni biashara au
mradi fulani, lakini katika hali ya kushangaza analiacha jambo lile na
kudai kwamba atalifanya muda mwingine. Kuahirisha mambo kwa namna hiyo
kunavyoendelea kwa muda ndivyo ambavyo hujikuta ndoto na mafanikio ya
wengi hufia hapo.
Fanya
maamuzi sahihi katika wakati ulionao maana hakuna wakati mwingine
utakuwa na nafuu ya kufanya unachotaka kufanya maana kila siku inakuja
na mambo mengine. Na kadiri utakavyokuwa unaahirisha mambo ndivyo
unavyochelewesha mafanikio yako na muda ndivyo unavyokwenda.
Kama
unataka kutimiza malengo yako epuka sana tabia hii maana ni matokeo ya
woga. Mtu mwoga hawezi kutimiza malengo yake kwa wakati.
"Woga wako ni umaskini wako". Woga kwenye maisha unafanya mtu anakuwa maskini au anarudi nyuma kwa sababu kila kitu anakiona ni kigumu. Utaona watu wanafanikiwa, wanafanya mambo yao yanaenda vizuri kwa sababu wamethubutu na kuchukua hatua wakati wewe unasubiri hali iwe nzuri mwisho wake utaishia kujilaumu kwa sababu utakuwa umechelewa au ukashindwa kabisa.
Wakati
sahihi ndio huu, simamia unachokiamini na weka woga pembeni uanze
kufanyia kazi wazo lako huku ukimwomba Mungu, utafanikiwa.
Naamini sasa kupitia somo hili fupi umeweza kubadili mtazamo wako na kama ulikuwa na tabia hii ya kuahirisha mambo, utaiacha na kusonga mbele.
Nakutakia mafanikio mema wakati unapoanza kuchukua hatua kwa ujasiri na kufanyia kazi ndoto zako.
Ni mimi rafiki yako,
Innocent Moshi
0658 185 444/ 0625 695 550
E-mail: innommoja2@gmail.com
Comments
Post a Comment