NI KWA NINI MAONO YAKO HAYAFANIKIWI?
Ndugu msomaji wa makala hii, huenda umewahi kujiuliza ni kwa nini unakuwa na maono lakini hayfanikiwi au hayatimii. Leo nataka tuzunguze kwa habari ya madhara yatokanayo na kuwaambia watu maono uliyo nayo kabla ya kuyaweka katika vitendo. Tutajifunza nini maana ya maono, faida ya kuwa na maono lakini pia tutajifunza madhara yatokanayo na kuwaambia watu maono yako kabla hayajatimia au hujayafanyia kazi. Nini maana ya maono? Yamkini umesikia hili neno maono lakini hujapata maana yake kamili. Maono ni picha ya mbeleni, malengo na mipango ambayo mtu anakuwa nayo na, ambayo atafanyia juhudi ili afikie au atimize. Malengo au mipango mtu anaipanga kwa siku zijazo au wakati fulani ulioko mbeleni ili kutekeleza, tunaweza kuichukulia kama maono mtu aliyo nayo. Kwa mfano, unataka baada ya miezi sita uwe na kiwanja cha kujenga nyumba au uwe na gari lako mwenyewe, hayo ni maono ambayo unatamani yatimie katika wakati huo. Hivyo tunaweza kusema kuwa hiyo ni picha yako ya mbe...